0:00
0:00

Mlango 93

Bwana ametamalaki, amejivika adhama, Bwana amejivika, na kujikaza nguvu. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;
2 Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani; Wewe ndiwe uliye tangu milele.
3 Ee Bwana, mito imepaza, Mito imepaza sauti zake, Mito imepaza uvumi wake.
4 Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu, Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo, Bwana Aliye juu ndiye mwenye ukuu.
5 Shuhuda zako ni amini sana; Utakatifu ndio uifaao nyumba yako, Ee Bwana, milele na milele.