0:00
0:00

Mlango 82

Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu; Katikati ya miungu anahukumu.
2 Hata lini mtahukumu kwa dhuluma, Na kuzikubali nyuso za wabaya?
3 Mfanyieni hukumu maskini na yatima; Mtendeeni haki aliyeonewa na fukara;
4 Mwokoeni maskini na mhitaji; Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.
5 Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani; Misingi yote ya nchi imetikisika.
6 Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia.
7 Lakini mtakufa kama wanadamu, Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.
8 Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi, Maana Wewe utawarithi mataifa yote.