Kujitenga kutoka kwa wapendwa

0:00
0:00

 • na Mispa, maana alisema, Mungu avizie kati ya mimi na wewe, wakati tusipoonana.
  Mwanzo 31:49
 • Naliomba nipewe mtoto huyu; Bwana akanipa dua yangu niliyomwomba; kwa sababu hiyo mimi nami nimempa Bwana mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa Bwana. Naye akamwabudu Bwana huko.
  1 Samweli 1:27, 28
 • Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
  Zaburi 23:4
 • Baba yangu na mama yangu wameniacha, Bali Bwana atanikaribisha kwake.
  Zaburi 27:10
 • Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa.
  Zaburi 34:18
 • Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuziganga jeraha zao.
  Zaburi 147:3
 • Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, Wala mito haiwezi kuuzamisha; Kama mtu angetoa badala ya upendo Mali yote ya nyumbani mwake, Angedharauliwa kabisa.
  Wimbo Ulio Bora 8:7
 • Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.
  Yohana 14:18
 • Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu.
  Warumi 8:18
 • atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu.
  2 Wakorintho 1:4
 • Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;
  Wafilipi 3:7, 8
 • Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.
  1 Wathesalonike 4:13
 • ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.
  1 Petro 1:7
 • Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi.
  Waebrania 10:36