Kiburi

0:00
0:00

  • Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani.
    1 Samweli 2:3
  • Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu.
    Mithali 11:2
  • Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.
    Mithali 13:10
  • Bwana ataing'oa nyumba ya mwenye kiburi; Bali atauthibitisha mpaka wa mjane.
    Mithali 15:25
  • Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha Bwana Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima.
    Mithali 22:4
  • Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa.
    Mithali 29:23
  • Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.
    1 Wakorintho 10:12
  • Na torati haikuja kwa imani, bali, Ayatendaye hayo ataishi katika hayo.
    Wagalatia 3:12
  • Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.
    Yakobo 4:10
  • Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
    Luka 14:11
  • Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
    Wagalatia 5:22, 23
  • Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
    Wafilipi 2:3-5
  • Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa Bwana; Hakika, hatakosa adhabu.
    Mithali 16:5
  • Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.
    Mithali 16:18
  • Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti.
    Mithali 16:25
  • Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.
    Mithali 18:12
  • Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.
    Yakobo 4:6
  • Wenye upole atawaongoza katika hukumu, Wenye upole atawafundisha njia yake.
    Zaburi 25:9
  • Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema. Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
    1 Petro 5:5-7
  • Mfalme wa Israeli akajibu, akasema, Mwambieni, Avaaye asijisifu kama avuaye.
    1 Wafalme 20:11
  • Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.
    Isaya 66:2