Wanategemea tu juu ya Bwana

0:00
0:00

 • Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya. Kutoka 14:13, 14
 • Utokapo kwenda vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi, na magari, na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope; kwa kuwa Bwana Mungu wako, yu pamoja nawe, aliyekukweza kutoka nchi ya Misri. Kumbukumbu la Torati 20:1
 • Naye Bwana, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike. Kumbukumbu la Torati 31:8
 • Mtu mmoja miongoni mwenu atafukuza watu elfu; maana Bwana, Mungu wenu, ndiye anayewapigania, kama alivyowaambia. Yoshua 23:10
 • Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda; 1 Samweli 2:9
 • Basi, Yonathani akamwambia yule kijana aliyemchukulia silaha zake, Haya! Na twende tukawavukie ngomeni hao wasiotahiriwa; yamkini Bwana atatutendea kazi; kwa maana hakuna la kumzuia Bwana asiokoe, kwamba ni kwa wengi au kwamba ni kwa wachache. 1 Samweli 14:6
 • Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu. 1 Samweli 17:47
 • Iweni hodari, na wa moyo mkuu, msiogope, wala msifadhaike kwa sababu ya mfalme wa Ashuru, wala kwa majeshi yote walio pamoja naye; kwa maana yupo mkuu pamoja nasi kuliko aliye pamoja naye; kwake upo mkono wa mwili; ila kwetu yupo Bwana, Mungu wetu, kutusaidia, na kutupigania mapigano yetu. Na watu wakayategemea maneno ya Hezekia, mfalme wa Yuda. 2 Mambo ya Nyakati 32:7, 8
 • Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako, Hatua zangu hazikuondoshwa. Zaburi 17:5
 • Ee Bwana, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini Bwana bila wasiwasi. Zaburi 26:1
 • Utuletee msaada juu ya mtesi, Maana wokovu wa binadamu haufai. Zaburi 60:11
 • Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa kimya. Tumaini langu hutoka kwake. Zaburi 62:5
 • Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako, Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake. Wakipita kati ya bonde la Vilio, Hulifanya kuwa chemchemi, Naam, mvua ya vuli hulivika baraka Huendelea toka nguvu hata nguvu, Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu. Zaburi 84:5, 7
 • Hataogopa habari mbaya; Moyo wake u imara ukimtumaini Bwana. Moyo wake umethibitika hataogopa, Hata awaone watesi wake wameshindwa. Zaburi 112:7, 8
 • It is better to trust in the LORD than to put confidence in man. Zaburi 118:8
 • Ni heri kumkimbilia Bwana Kuliko kuwatumainia wanadamu. Zaburi 143:8
 • Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. Mithali 3:5, 6
 • Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali. Isaya 30:15
 • Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi. Zekaria 4:6
 • Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. Yohana 15:5
 • Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. 1Yohana 5:4