Kwa sauti yake, naye Jibu

0:00
0:00

  • Njoni, enyi wana, mnisikilize, Nami nitawafundisha kumcha Bwana. [Zaburi 34:11]
  • Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako. [Zaburi 119:9]
  • Bwana atanitimilizia mambo yangu; Ee Bwana, fadhili zako ni za milele; Usiziache kazi za mikono yako. [Zaburi 138:8]
  • Wana wetu na wawe kama miche Waliokua ujanani. Binti zetu kama nguzo za pembeni Zilizonakishwa kwa kupamba hekalu. [Zaburi 144:12]
  • Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. [Mithali 3:1]
  • Basi, wanangu, nisikilizeni sasa; Maana heri hao wazishikao amri zangu. Sikieni mafundisho, mpate hekima, Wala msiikatae. [Mithali 8:32-33]
  • Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee. [Mithali 22:6]
  • Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi. [Isaya 54:13]
  • Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia , Naam ,Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu. [Yohana 21:15]
  • Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi. [2 Timotheo 2:22]
  • Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli. [3Yohana 1:4]
  • Kwa kuwa Bwana ampendaye humrudi, Kama vile baba mwanawe ampendezaye. [Mithali 3:12]
  • Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema. [Mithali 13:24]
  • Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini; Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake. [Mithali 19:18]
  • Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali. [Mithali 22:15]
  • Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. [Mithali 23:13]
  • Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa. [Wakolosai 3:21]
  • mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; [1 Timotheo 3:4]
  • tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye; Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? [Waebrania 12:5-9]
  • nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. [Kumbukumbu la Torati 6:7]
  • Maneno haya nikuagizayo yote yatunze na kuyasikiza, ili upate kufanikiwa na watoto wako baada yako milele, hapo uyafanyapo yaliyo mema na kuelekea machoni pa Bwana, Mungu wako. [Kumbukumbu la Torati 12:28]
  • akawaambia, Yawekeni mioyoni mwenu maneno yote ambayo nashuhudia kwenu hivi leo; nayo waamuruni watoto wenu, wayatunze na kuyafanya maneno yote ya torati hii. Kwa maana si jambo lisilofaa kwenu; maana, ni maisha yenu, na kwa jambo hili mtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki. [Kumbukumbu la Torati 32:46, 47]
  • Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi. Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau; Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu. [Mithali 4:4,5]
  • Mwenye haki aendaye katika unyofu wake, Watoto wake wabarikiwa baada yake. [Mithali 20:7]
  • Nikatazama, nikaondoka, nikawaambia wakuu, na mashehe, na watu wengine waliobaki, Msiwaogope; mkumbukeni Bwana, aliye mkuu mwenye kuogofya, mkawapiganie ndugu zenu, na wana wenu, na binti zenu, na wake zenu, na nyumba zenu. [Nehemia 4:14]
  • Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana. [Waefeso 6:4]
  • Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine. [2 Timotheo 2:2]