Mstari wa Siku
[Copy and send, from here:]
Mstari wa Siku:
Habari za asubuhi! 🙂
https://www.wordproject.org/bibles/votd3/index_sw.htm
Mistari ya kila mwezi ya Biblia:
Day 1
"Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo; sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje.Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu.
- Yohana 12:31-32
Day 2
"Heri aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake, Wala hakuwaelekea wenye kiburi, Wala hao wanaogeukia uongo.
- Zaburi 40:4
Day 3
"Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.
- Mithali 3:5,6
Day 4
"Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.
- Isaya 65:24
Day 5
"Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu.Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.
- Yakobo 4:8-10
Day 6
"Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote.
- 1 Wakorintho 6:12
Day 7
"Basi, wataliogopa jina la Bwana toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya Bwana
- Isaya 59:19
Day 8
"Hakuna aliye mtakatifu kama Bwana; Kwa maana hakuna ye yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani.
- 1 Samweli 2:2-3
Day 9
"Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
- Mwanzo 2:24
Day 10
"Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.-
- Ufunuo wa Yohana 12:7-8
Day 11
"Lakini Yesu akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu; wala msiwazuie; kwa maana walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao.
- Mathayo 19:14
Day 12
"Bwana, asubuhi utaisikia sauti yangu, Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.
- Zaburi 5:3
Day 13
"Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.;
- 1 Petro 2:11
Day 14
"Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo.
- 2 Yohana 2:6
Day 15
"Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
- Mathayo 4:17
Day 16
"Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga.
- Zaburi 119:130
Day 17
"Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
- Yohana 1:12-13
Day 18
"Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
- Wakolosai 2:16-17
Day 19
"Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.
- Mathayo 22:36-40
Day 20
"jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.
- Isaya 1:17
Day 21
"Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, Atajilinda nafsi yake na taabu.
- Mithali 21:23
Day 22
"Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu;huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.
- Warumi 4:20, 21
Day 23
"ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana;ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.
- 1 Timotheo 6:15-16
Day 24
"
"Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
- Waebrania 11:1
Day 25
"Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote;
- 2 Wakorintho 1:3
Day 26
"Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia.
- Zaburi 5:11
Day 27
"Mataifa yote huwa kama si kitu mbele zake; huhesabiwa kwake kuwa duni ya si kitu, na ubatili.
- Isaya 40:17
Day 28
"na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.
- 1 Yohana 3:22
Day 29
" Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
- Warumi 10:17