Mstari wa Siku

[Copy and send, from here:]

Mstari wa Siku:

Habari za asubuhi! 🙂

https://www.wordproject.org/bibles/votd2/index_sw.htm


Mistari ya kila mwezi ya Biblia:

Oct. 1
"Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
- Yohana 15:5

Oct. 2
"Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa; twaudhiwa, bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi;
- 2 Wakorintho 4:8,9

Oct. 3
"Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
- Yakobo 1:5

Oct. 4
"Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
- 2 Timotheo 1:7

Oct. 5
"Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
- 1 Yohana 1:8,9

Oct. 6
"Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.
- Yakobo 4:10

Oct. 7
"Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi.
- Waebrania 10:36

Oct. 8
"MMfanyieni Bwana shangwe, dunia yote; Mtumikieni Bwana kwa furaha; Njoni mbele zake kwa kuimba;
- Zaburi 100:1,2

Oct. 9
"Njia za mtu zikimpendeza Bwana, Hata adui zake huwapatanisha naye.
- Mithali 16:7

Oct. 10
"Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.
- Yohana 14:27

Oct. 11
"Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,
- Warumi 5:1

Oct. 12
"Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake.
- Waebrania 4:9,10

Oct. 13
"wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;
- Warumi 3:23

Oct. 14
"Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;
- Isaya 55:6

Oct. 15
"Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu.
- Ufunuo wa Yohana 19:5

Oct. 16
"Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.
- Yakobo 2:26

Oct. 17
"Bwana atawapa watu wake nguvu; Bwana atawabariki watu wake kwa amani.
- Zaburi 29:11

Oct. 18
"huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
- 1 Petro 5:7

Oct. 19
"Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
- Waebrania 4:12

Oct. 20
"Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.
- 1 Yohana 4:18

Oct. 21
"Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.
- Wafilipi 4:19

Oct. 22
"Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote za maisha yako ya ubatili, ulizopewa chini ya jua; siku zote za ubatili wako, kwa maana huo ni sehemu yako ya maisha; na katika taabu zako ulizozitaabika chini ya jua.
- Mhubiri 9:9

Oct. 23
"Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;
- Wafilipi 1:6

Oct. 24
"tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
- Waefeso 4:32

Oct. 25
"mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.
- Waebrania 12:13

Oct. 26
"Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
- Waefeso 6:12

Oct. 27
"Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
- Warumi 14:17

Oct. 28
"Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
- Ufunuo wa Yohana 12:11

Oct. 29
"bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
- Isaya 40:31

Oct. 30
"Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
- Yohana 1:3

/*October has 31 days*/

Oct. 31
"Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
- Yakobo 5:16