Mstari wa Siku

[Copy and send, from here:]

Mstari wa Siku:

Habari za asubuhi! 🙂

https://www.wordproject.org/bibles/votd/index_sw.htm


Mistari ya kila mwezi ya Biblia:

Day 1
"Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote.
- Zaburi 34:19

Day 2
"Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
- Mathayo 27:46

Day 3
" Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.
- Yohana 12:24

Day 4
"Naye akawaambia, Msistaajabu; mnamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulibiwa; amefufuka; hayupo hapa; patazameni mahali walipomweka.
- Marko 16:6

Day 5
"Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
- 1 Yohana 1:9

Day 6
"...na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
- Mathayo 16:18

Day 7
"Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.
- Zaburi 16:11

Day 8
"...Uwe hodari, mwenye moyo mkuu, ukatende hivyo; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu, Mungu wangu, yu pamoja nawe; ...
- 1 Mambo ya Nyakati 28:20

Day 9
"Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, ...Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
- Mwanzo 1:21

Day 10
"Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
- Yohana 15:7

Day 11
"Kwa kuwa Bwana ampendaye humrudi, Kama vile baba mwanawe ampendezaye.
- Mithali 3:12

Day 12
"Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.
- Yohana 16:24

Day 13
"Utabarikiwa kuliko mataifa yote; hakutakuwa na mtu mume wala mke aliye tasa kati yenu; wala kati ya wanyama wenu wa mifugo.
- Kumbukumbu la Torati 7:14

Day 14
"Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe, Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.
- Zaburi 98:1

Day 15
"Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
- Warumi 12:18

Day 16
"Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama.
- Zaburi 4:8

Day 17
"Naye Bwana, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike.
- Kumbukumbu la Torati 31:8

Day 18
" Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.
- Yohana 8:36

Day 19
"Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
- Mithali 28:13

Day 20
"zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
- Waefeso 6:16

Day 21
"Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
- Yohana 14:6

Day 22
"Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu.
- Mithali 11:2

Day 23
"Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
- Zaburi 23:4

Day 24
"Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
- Yakobo 3:17

Day 25
"wakiwaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu, maana mtu akishindwa na mtu huwa mtumwa wa mtu yule.
- 2 Petro 2:19

Day 26
"...na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
- Mathayo 16:19

Day 27
"Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.
- Kutoka 23:20

Day 28
"akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
- Mathayo 19:5

Day 29
"Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,
- 1 Wakorintho 2:4

Day 30
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. -
- Yohana 3:16