Hekima na maamuzi
- akawaambia hao makadhi, Angalieni myafanyayo; kwa kuwa hammfanyii mwanadamu hukumu, ila Bwana; naye yupo pamoja nanyi katika neno la hukumu.
2 Mambo ya Nyakati 19:6 -
Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu; Ndipo utakapofahamu kumcha Bwana, Na kupata kumjua Mungu. Kwa kuwa Bwana huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;
Mithali 2:3, 5, 6 -
Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana.
Mithali 16:1 -
Watu wabaya hawaelewi na hukumu; Bali wamtafutao Bwana huelewa na yote.
Mithali 28:5 -
Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana; na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;
Isaya 11:2, 3 -
Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieliii naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.
Danieli 1:17 -
Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
Yakobo 1:5 -
Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unijulishe njia nitakayoiendea, Kwa maana nakuinulia nafsi yangu.
Zaburi 143:8 -
Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa, Ee Bwana, unihuishe kwa ajili ya jina lako, Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni;
Zaburi 143:10, 11 -
mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.
Mithali 1:5 -
Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe; Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri.
Mithali 12:15 -
Pasipo mashauri makusudi hubatilika; Bali kwa wingi wa washauri huthibithika.
Mithali 15:22 -
Sikiliza mashauri, ukapokee mafundisho, Upate kuwa na hekima siku zako za mwisho.
Mithali 19:20 -
Kila kusudi huthibitika kwa kushauriana; Na kwa shauri la akili fanya vita.
Mithali 20:18 -
Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu.
Mithali 24:6 -
Basi msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki.
Yohana 7:24 -
Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
Yakobo 3:17 -
Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa.
2 Wakorintho 13:1