Uaminifu

0:00
0:00

 • Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake;
  Wakolosai 3:9
 • Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.
  Warumi 12:17
 • tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya wanadamu.
  2 Wakorintho 8:21
 • Mizani ya hadaa ni chukizo kwa Bwana; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza.
  Mithali 11:1, 3
 • Katika kosa la midomo kuna mtego kwa mbaya; Bali mwenye haki atatoka katika taabu. Atamkaye maneno ya kweli hufunua haki; Bali shahidi wa uongo hutamka hila.
  Mithali 12:13, 17
 • Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
  Mithali 28:13
 • Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
  Yakobo 5:16
 • lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu.
  2 Wakorintho 4:2