Furaha

0:00
0:00

  • Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia.
    Zaburi 5:11
  • Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.
    Zaburi 16:11
  • Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, Katika radhi yake mna uhai. Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha.
    Zaburi 30:5
  • Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha.
    Zaburi 126:5
  • Heri kila mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake. Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema.
    Zaburi 128:1, 2
  • Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.
    Isaya 35:10
  • Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.
    Yohana 15:11
  • Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
    Warumi 14:17