Usalama wa Ulinzi na adui

0:00
0:00

 • Kwa sababu hii zitendeni amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzifanya; nanyi mtakaa katika hiyo nchi salama.
  MAMBO YA WALAWI 25:18
 • Akamnena Benyamini, Mpenzi wa Bwana atakaa salama kwake; Yuamfunika mchana kutwa, Naye hukaa kati ya mabega yake.
  KUMBUKUMBU LA TORATI 33:12
 • Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui; Akasema, Angamiza.
  KUMBUKUMBU LA TORATI 33:27
 • basi, sasa, uwe radhi, ukaibarikie nyumba ya mtumwa wako, ipate kudumu milele mbele zako; kwa maana wewe, Ee Bwana MUNGU, umelinena na kwa baraka yako nyumba ya mtumwa wako na ibarikiwe milele.
  2 SAMWELI 7:29
 • Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski, na hao Washami wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.
  2 SAMWELI 8:6
 • nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina, kama jina la hao wakuu walioko duniani.
  1 MAMBO YA NYAKATI 17:8
 • Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama.
  ZABURI 4:8
 • Nimemweka Bwana mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa.
  ZABURI 16:8
 • Kwa kuwa mfalme humtumaini Bwana, Na kwa fadhili zake Aliye juu hataondoshwa. Mkono wako utawapata adui zako wote, Mkono wako wa kuume utawapata wanaokuchukia. Utawafanya kuwa kama tanuru ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. Bwana atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawala.
  ZABURI 21:7-9
 • Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
  ZABURI 34:7
 • Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
  ZABURI 46:1
 • Bali mfalme atamfurahia Mungu, Kila aapaye kwa Yeye atashangilia, Kwa maana vinywa vya waongo vitafumbwa.
  ZABURI 63:11
 • Kwa kuwa Wewe Bwana ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako. Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.
  ZABURI 91:9, 10
 • Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure.
  ZABURI 127:1
 • Hapo nitamchipushia Daudi pembe, Na taa nimemtengenezea masihi wangu. Adui zake nitawavika aibu, Bali juu yake taji yake itasitawi.
  ZABURI 132:17,18
 • Awapaye wafalme wokovu, Amwokoa Daudi, mtumishi wake, na upanga wa uovu.
  ZABURI 144:10
 • Kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako, Naye atakulinda mguu wako usinaswe.
  MITHALI 3:26
 • Kumcha Bwana ni tumaini imara; Watoto wake watakuwa na kimbilio.
  MITHALI 14:26
 • Jina la Bwana ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.
  MITHALI 18:10
 • Farasi huwekwa tayari kwa siku ya vita; Lakini Bwana ndiye aletaye wokovu.
  MITHALI 21:31
 • Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio.
  MITHALI 30:5
 • Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.
  AMOSI 3:7
 • Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
  WAEFESO 6:11, 12