Kupumzika katika Bwana

0:00
0:00

  • Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.
    Kutoka 33:14
  • Hata walipokuwa wakishuka mwisho wa mji, Samweli akamwambia Sauli, Mwambie mtumishi atangulie, (naye akatangulia), bali wewe simama hapa sasa, ili nikuambie neno la Mungu.
    1 Samweli 9:27
  • Naye akawaambia Yuda, Na tuijenge miji hii, na kuizungushia maboma, na minara, na malango, na makomeo; nchi bado ikalipo mbele yetu, kwa kuwa tumemtafuta Bwana, Mungu wetu; naam, tumemtafuta, naye amemstarehesha pande zote. Basi wakajenga, wakafanikiwa.
    2 Mambo ya Nyakati 14:7
  • Mwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.
    Zaburi 4:4
  • Umngoje Bwana, uwe hodari, Upige moyo konde, naam, umngoje Bwana.
    Zaburi 27:14
  • Ukae kimya mbele za Bwana, Nawe umngojee kwa saburi; Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu afanyaye hila.
    Zaburi 37:7
  • Nalimngoja Bwana kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu.
    Zaburi 40:1
  • Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.
    Zaburi 46:10
  • Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.
    Zaburi 55:22
  • Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu.
    Zaburi 62:8
  • Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.
    Isaya 26:3
  • Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali.
    Isaya 30:15
  • Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima.
    Isaya 32:17
  • bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
    Isaya 40:31
  • Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.
    Yeremia 17:7
  • Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.
    Yeremia 29:11
  • Bwana ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo. Ni vema mtu autarajie wokovu wa Bwana Na kumngojea kwa utulivu.
    Maombolezo 3:25, 26
  • Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
    Mathayo 11:28-30
  • Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
    Wafilipi 4:7
  • Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, wala sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile.
    2 Timotheo 1:12
  • huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
    1 Petro 5:7