Sifa

0:00
0:00

 • Kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu.
  Nehemia 8:10
 • Nitamhimidi Bwana kila wakati, Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
  Zaburi 34:1
 • Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.
  Zaburi 50:23
 • Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake. Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi; Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi; Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana. Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.
  Zaburi 150
 • Heri watu wale waijuao sauti ya shangwe, Ee Bwana, huenenda katika nuru ya uso wako.
  Zaburi 89:15
 • Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote; Mtumikieni Bwana kwa furaha; Njoni mbele zake kwa kuimba;
  Zaburi 100:1, 2
 • Ni neno jema kumshukuru Bwana, Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu.
  Zaburi 92:1
 • Rehema na hukumu nitaziimba, Ee Bwana, nitakuimbia zaburi.
  Zaburi 101:1
 • Bwana ametamalaki, nchi na ishangilie, Visiwa vingi na vifurahi.
  Zaburi 97:1
 • Enyi wenye haki, mmfurahieni Bwana, Na kulishukuru jina lake takatifu.
  Zaburi 97:12
 • Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote.
  Zaburi 103:1, 2
 • Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa matari na kinubi wamwimbie. Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu. Watauwa na waushangilie utukufu, Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.
  Zaburi 149:1, 3-5
 • Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.
  Zaburi 50:23
 • Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.
  Matendo ya Mitume 16:25
 • Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia Bwana, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni Bwana; kwa maana fadhili zake ni za milele. Nao walipoanza kuimba na kusifu, Bwana akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa.
  2 Mambo ya Nyakati 20:21, 22
 • shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
  1 Wathesalonike 5:18
 • Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake.
  Waebrania 13:15
 • Kinywa changu kitajazwa sifa zako, Na heshima yako mchana kutwa.
  Zaburi 71:8
 • Nami nitatumaini daima, Nitazidi kuongeza sifa zake zote.
  Zaburi 71:14
 • Toka maawio ya jua hata machweo yake Jina la Bwana husifiwa.
  Zaburi 113:3
 • mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;
  Waefeso 5:19, 20
 • Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu.
  Ufunuo wa Yohana 19:5