Mstari wa Siku

[Copy and send, from here:]

Mstari wa Siku:

Habari za asubuhi! 🙂

https://www.wordproject.org/bibles/votd3/index_sw.htm


Mistari ya kila mwezi ya Biblia:

Day 1
"Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake;mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba.
- Wakolosai 3:9-10

Day 2
"Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
- Ufunuo wa Yohana 3:21

Day 3
"Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.
- Mithali 3:5, 6

Day 4
"Ni heri kumkimbilia Bwana Kuliko kuwatumainia wanadamu.
- Zaburi 118:8

Day 5
"Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.
- 1 John 1:9-10

Day 6
"Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
- Mathayo 16:26

Day 7
"Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.
- Zaburi 16:11

Day 8
" Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.
- Wafilipi 2:13

Day 9
" Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
- Mwanzo 1:21

Day 10
"Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
- Yohana 15:7

Day 11
"Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu.
- Mithali 11:2

Day 12
"Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.
- Yohana 16:24

Day 13
"Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.
- Yohana 12:24

Day 14
" Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo
- Waebrania 12:14-15

Day 15
"Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
- Warumi 12:17-18

Day 16
"Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama.
- Zaburi 4:8

Day 17
"Naye Bwana, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike.
- Kumbukumbu la Torati 31:8

Day 18
"Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.
- Yohana 8:36

Day 19
"akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
- Mathayo 19:5,6

Day 20
"zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
- Waefeso 6:16

Day 21
"Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
- Yohana 14:6

Day 22
"Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.
- Ufunuo wa Yohana 2:7

Day 23
"Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
- Zaburi 23:4

Day 24
"Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
- Yakobo 3:17

Day 25
"wakiwaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu, maana mtu akishindwa na mtu huwa mtumwa wa mtu yule.
- 2 Petro 2:19

Day 26
"Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.
- 1 Petro 1:13

Day 27
"Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.
- Kutoka 23:20

Day 28
"Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
- Mithali 28:13

Day 29
"Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,
- 1 Wakorintho 2:4

Day 30
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. -
- Yohana 3:16